Virusi vya korona ni jamii kubwa ya virusi vinavyojulikana kusababisha magonjwa yanayoanzia homa ya kawaida hadi homa kali kama vile Homa Kali ya Upumuaji ya Mashariki ya Kati (MERS) na Homa Kali ya Mfumo wa Upumuaji (SARS).
Virusi vipya vya korona (COVID-19) viligunduliwa 2019 huko Wuhan, China. Hivi ni virusi vipya vya korona ambavyo havijatambuliwa hapo awali kwa wanadamu.
Kozi hii hutoa utangulizi wa jumla wa COVID-19 na virusi vinavyoibuka vya mfumo wa upumuaji na inawelenga wataalamu wa afya ya umma, wasimamizi wa majanga na wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa, mashirika ya kimataifa na Mashirika yasiyo ya Kiserikali.
Kama ilivyo jina rasmi la ugonjwa lilianzishwa baada ya kuundwa kwa nyenzo, mtajo wowote wa nCoV unahusu COVID-19, ugonjwa ambukizi unaosababishwa na virusi vya korona vilivyoguduliwa hivi karibuni.
Kozi hii pia inapatikana katika lugha zifuatazo:
English - français - Español - 中文 - Português - العربية - русский - Türkçe - српски језик - فارسی - हिन्दी, हिंदी - македонски јазик - Tiếng Việt - Indian sign language - magyar - Bahasa Indonesia - বাংলা - اردو - አማርኛ - ଓଡିଆ - Hausa - Tetun - Deutsch - Èdè Yorùbá - Asụsụ Igbo - ਪੰਜਾਬੀ - isiZulu - Soomaaliga - Afaan Oromoo - دری - Kurdî - پښتو - मराठी - Fulfulde- සිංහල - Latviešu valoda
Muhtasari:
Kozi hii inatoa utangulizi wa jumla wa virusi vinavyoibuka vya mfumo wa kupumua, ikiwemo virusi vipya vya korona. Kufikia mwisho wa kozi hii, utakuwa na uwezo wa kuelezea:
Kuna rasilimali zilizowekwa kwenye kila moduli kukusaidia kuelewa zaidi mada hii.
Lengo la kujifunza: Fafanua kanuni za msingi za virusi vinavyojitokeza vya mfumo wa kupumua na jinsi ya kushughulikia mlipuko kwa ufanisi.
Muda wa kozi: Takriban masaa 3.
Vyeti: Rekodi ya cheti cha Mafanikio itapatikana kwa washiriki ambao alama angalau 80% ya jumla ya alama zinazopatikana katika majibu yote.
Imetafsiriwa kwa Kiswahili kutoka Emerging respiratory viruses, including COVID-19: methods for detection, prevention, response and control, 2020. WHO halijukumiki kwa yaliyomo au usahihi wa tafsiri hii. Katika tukio la kutokubaliana lolote kati ya Kiingereza na tafsiri ya Kiswahili, toleo la asili la Kiingereza litakuwa toleo la kufuatwa na toleo halisi.
Tafsiri hii haijathibitishwa na WHO. Nyenzo hii imekusudiwa kwa madhumuni ya msaada wa kujifunza tu.