There is no public course content yet.

Course is available

Afya na usalama mahala pa kazi kwa wafanyakazi wa huduma za afya katika muktadha wa Korona (COVID-19)

Offered by OpenWHO
Afya na usalama mahala pa kazi kwa wafanyakazi wa huduma za afya katika muktadha wa Korona (COVID-19)

Wafanyakazi wote wa huduma za afya wanahitaji taaluma na ujuzi wa kujilinda pamoja na kuwalinda wengine dhidi ya vihatarishi vya mahala pa kazi wanavyokumbana navyo, ili waweze kufanya kazi kwa usalama na ufanisi.

Katika kukidhi mahitaji hayo, kozi hii itakuwa na jumla ya sehemu tano:
• Utangulizi
• Moduli ya 1: Vihatarishi vya maambukizi kwa afya na usalama
• Moduli ya 2: Hatari za kimwili kwa afya na usalama
• Moduli ya 3: Hatari za kisaikojamii kwa afya na usalama
• Moduli ya 4: Misingi ya afya na usalama mahala pa kazi katika huduma za afya.

Tafadhali kumbuka: Nyenzo hizi zilizinduliwa mnamo 21/08/2020.

Photo credit: WHO/P.Phutpheng

Nyenzo hizi zilizinduliwa tarehe 31/08/2020. Kwa vile ushahidi wa kisayansi na mwongozo wa kiufundi kuhusu COVID-19 unazidi kubadilika, tafadhali rejelea https://www.who.int/emergencies/diseases/novel-coronavirus-2019 kwa masasisho mapya zaidi.

Self-paced
Language: Kiswahili
COVID-19

Course information

Kozi hii pia inapatikana katika lugha zifuatazo:

English - македонски - Português - Español -Bahasa Indonesia - Nederlands - 日本語 - Казақ тілі - български - Français - Türkçe

Muhtasari: Katika muktadha wa janga la Korona (COVID-19), mazingira ya kazi ya wafanyakazi wa huduma za afya yanaweza kuwa mabaya. Pamoja na hatari ya kupata maambukizi, wafanyakazi wa huduma za afya wanaweza pia kukumbana na vihatarishi vya kibaiolojia, kimwili, au kisaikojamii. Kwa hiyo, katika kulinda ustawi wa kimwili na kiakili wa wafanyakazi wa huduma za afya, Shirika la Afya Dunia (WHO) limependekeza hatua kadhaa za kuchukuliwa ili kuzuia na kudhibiti maambukizi pamoja na msaada wa kuimarisha afya na usalama kazini, na saikolojiajamii.

Wafanyakazi wa huduma za afya wanaoshiriki katika mapambano ya janga la Korona wanakabiliwa na vihatarishi vingi kwa afya na usalama wao mahala pa kazi. Miongoni mwa vihatarishi hivyo ni kupata maambukizi ya COVID -19, kuumwa, na kusambaza maradhi kwa watu wengine; uchovu unaosababishwa na kufanya kazi kwa saa nyingi na wingi wa kazi, kutopata kulala au kupumzika vya kutosha, upungufu wa maji mwilini, lishe duni, majeraha ya misuli yanayosababishwa na ubebaji wa wagonjwa na vitu vyengine vizito, kufanya kazi kwa muda mrefu wakiwa wamevaa vifaa kinga ambavyo vinaweza kusababisha athari za joto, na kuathiri ngozi, vurugu na unyanyapaa kazini, na aina mbalimbali ya matatizo ya afya ya akili, msongo wa mawazo na kuchoshwa na kazi.

Walengwa wa kozi hii ni wafanyakazi wa huduma za afya, wasimamizi wa matukio ya dharura, wasimamizi wa kazi na viongozi wanaoandaa sera na itifaki kwa ajili ya vituo vyao vya kutolea huduma za afya.

Malengo ya somo: Mwisho wa somo, washiriki wanatarajiwa waweze:

● kueleza vihatarishi maarufu vya afya na usalama mahala pa kazi vinavyowakabili wafanyakazi wa huduma za afya wakati wa kupambana na janga la Korona - COVID-19;
● kueleza haki za wafanyakazi wa huduma za afya za kuwa na mazingira bora ya kazi;
● kueleza jinsi ya kuchukua hatua mbalimbali kwa ajili ya kulinda afya na usalama wao pamoja na kupendekeza namna ya kuimarisha hatua hizo; na
● kupata na kutumia huduma saidizi za kulinda afya na usalama kwa wafanyakazi wa huduma za afya.

Muda wa kozi: Kiasi cha saa 1

Vyeti: Cheti cha Ufaulu kitatolewa kwa kila mshiriki aliyefikia jumla ya 80% ya alama zinazotolewa kwa majaribio yote.. Washiriki wanaopokea Rekodi ya Mafanikio wanaweza pia kupakua Beji ya wazi kwa kozi hii. Bonyeza hapa kujifunza jinsi.

  Imetafsiriwa kwa Kiswahili kutoka Occupational health and safety for health workers in the context of COVID-19, 2020. WHO haliwajibiki kwa yaliyomo au usahihi wa tafsiri hii. Katika tukio la kutokubaliana lolote kati ya Kiingereza na tafsiri ya Kiswahili, toleo la asili la Kiingereza litakuwa toleo la kufuatwa na toleo halisi.

Course contents

  • Utangulizi:

    Moduli ya utangulizi inatoa muhtasari kuhusu afya na usalama mahala pa kazi katika muktadha wa Korona - COVID-19.
  • Moduli ya 1: Hatari za maambukizi kwa afya na usalama:

    Mwisho wa moduli hii unatarajiwa uweze; kufafanua kwa vipi maambuzi ya mfumo wa upumuaji na vimelea vilivyomo katika damu vinaweza kusambazwa kwa wafanyakazi wa afya; na kufafanua hatua ambazo wafanyakazi wa afya wanaweza kuchukua ili kujikinga na maambuziki ya mfumo wa upumuaji, kama vile kutumia tahadhari za kawaida na hatua za kudhibiti kuzuia maambukizi ya aina mbalimbali.
  • Moduli ya 2: Hatari za kimwili kwa afya na usalama:

    Mwisho wa moduli hii unatarajiwa uweze kuainisha mambo makuu yanayosababisha matatizo ya mifupa na misuli katika sekta ya afya; kueleza mambo hatarishi yanayofanyika wakati wa kuhudumia wagonjwa; na kueleza aina kuu za vihatarishi mahala pa kazi kazini ambavyo wafanyakazi wa huduma za afya wanakabiliana navyo na namna ya kuviepuka.
  • Moduli ya 3: Vihatarishi vya kisaikojamii kwa afya na usalama:

    Malengo ya Moduli hii ni pamoja na kuweza: kuorodhesha vyanzo vikuu vya vihatarishi vya kisaikojamii kwa wafanyakazi wa huduma za afya; kueleza dalili za uchovu na jinsi ya kuuepuka; kueleza vihatarishi, dalili na hatua za kuzuia vurugu pahala pa kazi; na pia kutambua vipi wafanyakazi wa huduma za afya na viongozi wanaweza kulinda na kusaidia afya ya akili ya wafanyakazi wa huduma za afya
  • Moduli ya 4: Misingi ya afya na usalama kazini katika huduma za afya:

    Mwisho wa Moduli hii, unatarajiwa uweze kueleza majukumu ya waajiri na viongozi katika kuhakikisha afya na usalama mahala pa kazi; lakini pia kueleza hatua zinazoweza kuchukuliwa na wafanyakazi wa huduma za afya katika maeneo ya kazi kuimarisha afya na usalama kazini.

Enroll me for this course

The course is free. Just register for an account on OpenWHO and take the course!
Enroll me now

Certificate Requirements

  • Gain a Record of Achievement by earning at least 80% of the maximum number of points from all graded assignments.
  • Gain an Open Badge by completing the course.