Course is available
Kozi hii inatanguliza Ugonjwa wa Virusi vya Marburg na kuainisha ishara, dalili, utambuzi, njia za maambukizi na epidemiolojia ya ugonjwa huo. Inajadili pia mikakati ya kuzuia na kudhibiti.
Shukrani kwa picha: Shirika la Afya Duniani (World Health Organization /WHO)/Christopher Black
Kozi hii pia inapatikana katika:
English - Français - Español - Dholuo - Kirundi
Maelezo ya jumla: Ugonjwa wa virusi vya Marburg ni ugonjwa unaosababishwa na wanyama wa pori ambao umesababisha milipuko kadhaa. Una uwezo wa kusababisha ugonjwa mbaya na kifo kwa wanadamu. Mapitio ya mwaka wa 2018 ya orodha ya Mpango wa WHO wa utafiti na maendeleo (research and development /R&D) ya magonjwa yaliyopewa kipaumbele inaonyesha kwamba kuna haja ya haraka ya kuharakishwa kwa utafiti na maendeleo ku husu virusi vya Marburg. Kozi hii ya utangulizi inatoa muhtasari wa ishara, dalili, njia za maambukizi, utambuzi, na epidemiolojia ya ugonjwa huo. Inajadili pia mikakati ya kuzuia na kudhibiti ugonjwa huo.
Malengo ya mafunzo: Mwishoni mwa kozi hii, washiriki wanapaswa kujua yafuatayo:
Muda wa Kozi: Takriban saa 1.
Vyeti: Uthibitisho wa Kushiriki unapatikana kwa washiriki wanaokamilisha asilimia 100 ya nyenzo za kozi.
Imetafsiriwa kwa Kiswahili kutoka Kiingereza Introduction to Marburg Virus Disease, 2021. WHO haiwajibiki kwa lolote kwa yaliyomo au usahihi wa tafsiri hii. Katika tukio la kutokubaliana kokote kati ya Kiingereza na tafsiri ya Kiswahili, toleo la asili la Kiingereza litakuwa toleo la kutegemewa na halali.
Tafsiri hii haijathibitishwa na WHO. Rasilimali hii imekusudiwa kwa madhumuni ya msaada wa kujifunza tu.