Curso disponível
Karibu kwenye kozi ya mtandaoni ya kiwango cha utangulizi kuhusu homa ya mgunda (leptospirosis), ugonjwa wa bakteria unoambukizwa kwa njia ya kugusana na wanyama jamii ya panya, wanyama wa nyumbani na maji machafu. Ugonjwa huu ni tatizo linaloibuka la afya ya jamii. Kozi hii ya kiwango cha utangulizi mtandaoni inalenga kuwapa maarifa ya kiwango cha utangulizi wahudumu walio mstari wa mbele katika kukabiliana ili kudhibiti milipuko ya homa ya mgunda (leptospirosis). Inatoa maarifa muhimu zaidi ya kisayansi, kiufundi na kiutendaji kupitia masomo ya video na vipimo vya kibinafsi.
Tafadhali kumbuka: Kozi hii ilitungwa mwaka 2018 na kuboreshwa upya tarehe 5 Juni 2023. Kwa taarifa za hivi karibuni, tafadhali rejelea mada husika za afya kwenye tovuti ya WHO.
Kozi hii pia inapatikana katika:
Maelezo ya jumla: Homa ya mgunda (Leptospirosis) ni ugonjwa wa wanyama na mazingira. Bakteria hutunzwa katika figo za wanyama kwa miezi na hata miaka, na bakteria hutolewa na wanyama hawa katika mazingira kwa njia ya mkojo. Maambukizi kwa binadamu husababishwa kwa kugusana na wanyama walio ambukizwa au maji machafu. Kuna sehemu tofauti za kuingilia za maambukizi haya, inaweza kuwa michubuko ya ngozi, inaweza kuwa kupitia utando wa kamasi, inaweza pia kutokea kupitia kuvuta hewa ya matone ya mkojo kwa mfano wakati wa shughuli za kilimo na wakati mwingine, hutokea kwa kunywa maji.
Kozi hii inatoa utangulizi wa jumla wa ugonjwa huu kupitia masomo yanayoweza kupakuliwa, nakala, na maswali ambayo yanaweza kupitiwa kwa uwezo wako mwenyewe.
Lengo la kujifunza: Mwishoni mwa kozi hii unapaswa kuwa na uwezo wa:
Tunatumaini kwamba kozi hii itakusaidia kubadili kile ulichokuwa unakijua mwanzo na kukusaidia kubadilisha kanuni bora juu ya udhibiti wa homa ya mgunda (leptospirosis) katika ukabilianaji.
Muda wa kozi: Takribani saa 1.
Vyeti: Uthibitisho wa Ushiriki unatolewa kwa washiriki ambao wanakamilisha angalau asilimia 80 ya nyenzo za kozi hiyo.